Klabu ya Real Madrid inaelezwa kupanga kuingia sokoni Januari kufanya usajili wa beki wa kulia ambapo inaonekana kutakua kuna pengo la muda mrefu la beki Dani Carvajal ambaye ataukosa msimu mzima.
Real Madrid mpango wao mkubwa ni kuhakikisha wanaingia sokoni kwenye dirisha dogo na kupata mbadala wa Dani Carvajal ambaye alipata majeraha katika mchezo wa ligi kuu ya Hispania dhidi ya Villarreal wikiendi iliyopita, Majeraha ambayo yanaelezwa ndio yatakua mwisho wa beki huyo kuonekana uwanjani msimu huu.Beki wa klabu ya Liverpool Trent Alexender Arnold ambaye hajasaini mkataba ndani ya klabu yake hiyo mpaka sasa anaelezwa yupo kwenye malengo ya muda mrefu ya mabingwa hao wa Ulaya, Huku ikielezwa ndio litakua chaguo lao wakiingia sokoni mwezi Januari kuhakikisha wananasa saini ya beki huyo.
Mpango mzito wa Real Madrid kama hawatafanikiwa kumpata Trent kwenye dirisha dogo ambaye yupo kwenye mipango yao ya muda mrefu watahakikisha wanampa mkataba wa awali ili wamsajili dirisha kubwa, Lakini mpango wa kwanza ni kuhakikisha wanapata mbadala wa Carvajal mpaka msimu huu umalizike.
This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.
Strictly Necessary Cookies
Strictly Necessary Cookie should be enabled at all times so that we can save your preferences for cookie settings.
If you disable this cookie, we will not be able to save your preferences. This means that every time you visit this website you will need to enable or disable cookies again.