Real Madrid Yaipasua Osasuna Vini Apiga Hattrick

Klabu ya Real Madrid baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo leo wamefanikiwa kupata matokeo ya ushindi katika mchezo wa ligi kuu ya Hispania wakiwa nyumbani dhidi ya klabu ya Osasuna.

Real Madrid walianza mchezo kwa kasi wakionekana wanataka kupata magoli ya mapema wakifanya mashambulizi mara kwa mara langoni mwa klabu ya Osasuna, Jitihada zao zililipa kwani mnamo dakika ya 34 Vinicius Jr alifunga bao la kwanza kuwatanguliza mabingwa hao watetezi wa La Liga kabla ya Bellingham kufunga bao la pili dakika ya 42 na mchezo kwenda mapumziko ubao ukisoma 2-0.real madridKipindi cha pili kilianza kwa kasi na vijana wa Carlo Ancelotti walionekana kuendelea kuhitaji kuongeza mtaji wa magoli kutokana na mashambulizi ambayo walikua wanafanya langoni kwa Osasuna, Ambapo dakika ya 61 Vinicius Jr alifunga bao lake la pili katika mchezo huo kabla ya kukamilisha Hattrick yake dakika ya 69.

Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Hispania klabu ya Real Madrid ambao wamekua hawana msimu mzuri mpaka sasa wamefanikiwa kufikisha alama 27 baada ya kucheza michezo 12 wakiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo nyuma ya mahasimu wao klabu ya Barcelona ambao ni vinara wakiwa na alama 33.

 

 

Acha ujumbe