Real Madrid Yaendelea Kuandamwa na Majeraha

Bundi anaendelea kuzunguka kwenye viunga vya Santiago Bernabeu ndio kauli ambayo unaweza kuitumia kwani klabu ya Real Madrid imekua ikiandamwa na majeraha kwa wachezaji wake haswa wachezaji waandamizi klabuni.

Leo Real Madrid imepata majeraha wengine watatu kwenye mchezo wa ligi kuu ya Hispania ambao walikua wanakipiga katika dimba lao Santiago Bernabeu dhidi ya klabu ya Osasuna, Ambapo wachezaji wake watatu walishindwa kumaliza hata kipindi cha kwanza katika mchezo huo.real madridEder Militao, Lucaz Vazquez, pamoja na Rodrygo Goes ni wachezaji ambao walishindwa kuendelea na mchezo wa leo kutokana na majeraha ambayo wameyapata katika mchezo huo, Huku hofu ikiwa kubwa zaidi kwa beki Eder Militao ambaye inaonekana jeraha linaweza kua kubwa na kumuweka nje kwa muda mrefu kama msimu uliomalizika.

Taarifa ya madaktari inasubiriwa kuthibitisha wachezaji hao wamepata majeraha ya aina gani na watakaa nje ya uwanja kwa kipindi gani, Mpaka sasa Real Madrid ina majeraha saba baada ya kuongezeka wacheaji watatu wa leo Dani Carvajal, Alaba, Courtois, Tchouameni, Rodrygo, Militao, pamoja na Vazquez.

Acha ujumbe