Real Madrid Wafungua Kesi ya Nidhamu Dhidi ya Valverde na Tchouameni

Klabu ya Real Madrid CF imetangaza rasmi kuanzisha uchunguzi wa kinidhamu dhidi ya viungo wake Federico Valverde na Aurelien Tchouameni kufuatia tukio kubwa lililotokea katika mazoezi ya timu hiyo siku ya Alhamisi.

Real Madrid Wafungua Kesi ya Nidhamu Dhidi ya Valverde na TchouameniKupitia taarifa rasmi iliyotolewa na klabu hiyo, Real Madrid ilieleza kuwa hatua hiyo imechukuliwa baada ya vurugu zilizotokea wakati wa mazoezi ya kikosi cha kwanza, huku uchunguzi wa ndani ukiendelea kabla ya kutolewa kwa adhabu yoyote.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

“Real Madrid CF inapenda kuwataarifu kuwa kufuatia matukio yaliyotokea katika mazoezi ya kikosi cha kwanza asubuhi ya leo, imeamuliwa kufunguliwa kwa taratibu za kinidhamu dhidi ya wachezaji wetu Valverde na Tchouameni,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Real Madrid Wafungua Kesi ya Nidhamu Dhidi ya Valverde na TchouameniVyombo mbalimbali vya habari nchini Hispania vimeripoti kuwa nahodha huyo wa Real Madrid, Valverde, alilazimika kupelekwa hospitali baada ya kuumia usoni kufuatia ugomvi na mwenzake Tchouameni wakati wa mazoezi hayo.

Real Madrid Wafungua Kesi ya Nidhamu Dhidi ya Valverde na TchouameniInaelezwa kuwa kiungo huyo wa kimataifa wa Uruguay alisindikizwa hospitali na kocha wa Real Madrid Alvaro Arbeloa kwa ajili ya kushonwa nyuzi kadhaa baada ya kupata majeraha ya usoni karibu na kituo cha mazoezi cha klabu hiyo.

Real Madrid Wafungua Kesi ya Nidhamu Dhidi ya Valverde na TchouameniKatika taarifa nyingine ya kitabibu, Real Madrid ilithibitisha kuwa Valverde amegundulika kupata majeraha ya kichwani baada ya kufanyiwa vipimo. “Valverde yupo nyumbani akiwa katika hali nzuri na anahitaji mapumziko ya siku 10 hadi 14 kulingana na maelekezo ya kitabibu,” ilieleza taarifa hiyo huku ikidaiwa kuwa wachezaji hao wawili walikuwa tayari wamezua mzozo mwingine siku moja kabla ya tukio hilo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.