Real Madrid Wanamvizia Trent

Klabu ya Real Madrid wanaelezwa kuanza mawindo kwa beki wa kulia wa klabu ya Liverpool raia wa kimataifa wa Uingereza Tren Alexender Arnold ambaye mkataba wake uko mbioni kumalizika.

Real Madrid wamefatilia mkataba wa Trent na wamegundua mkataba wa beki huyo mwenye ubora mkubwa unamalizika mwaka 2025, Hivo wao wameanza mchakato wa kuanza kuitafuta saini ya beki huyo ili aweze kujiunga na wababe hao wa soka kutoka nchini Hispania.real madridLicha ya mkataba wa beki Trent Alexender Arnold kuonekana uko mbioni kumalizika, Lakini klabu ya Liverpool mpaka sasa haijaanza mazungumzo ya kumpa mkataba beki huyo jambo ambalo limewapa ari miamba hiyo ya soka kutoka nchini Hispania.

Taarifa za ndani kutoka klabu ya Liverpool zinaeleza Vijogoo hao hawana mpango wa kumuuza mchezaji huyo kabisa, Kwani wanamuona beki huyo kama sura ya klabu yao na nahodha ajae ambapo kwasasa ni nahodha msaidizi hivo sio rahisi kumuachia.real madridUpande wa klabu ya Real Madrid wao wanaamini katika nguvu yao ya ushawishi sokoni kwani wachezaji wengi wanatamani kucheza klabu hiyo, Lakini pia wanaamini watatoa ofa nzuri ambayo itaweza kukiddhi matakwa ya klabu ya Liverpool na kumpata beki huyo.

Acha ujumbe