Aurélien Tchouaméni amekubali kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia Real Madrid hadi mwaka 2031, huku ripoti zikieleza kuwa mazungumzo yaliyohusisha uwezekano wa kujiunga na Manchester United hayakuwahi kufikia hatua ya karibu kutokana na masuala ya mshahara na msimamo wa Real Madrid kutokuwa tayari kumuachia.

Brahim Díaz, ambaye amekuwa katika kiwango bora akiitumikia Morocco kwenye Taji la Dunia kwa kutoa pasi nne za mabao, anapanga kubaki Real na kusaini mkataba mpya wa kuongeza muda wa kuendelea kuichezea klabu hiyo. Hatua hiyo inaungwa mkono na kocha José Mourinho licha ya kuvutiwa na klabu nyingine.
Tchouaméni pia amefikia makubaliano ya kuongeza mkataba wake na Real Madrid hadi mwaka 2031. Ripoti zinaeleza kuwa uvumi wa kuhamia Manchester United haukuwa na msingi mkubwa kwani tofauti ya maslahi ya kifedha pamoja na msimamo wa Madrid kutokubali kumuuza vilifanya dili hilo lisikaribie kutimia.
José Mourinho ameweka wazi malengo yake ya kuimarisha kikosi kwa kuwalenga beki Alessandro Bastoni, Tomas Araujo na kiungo wa Liverpool Alexis Mac Allister. Hata hivyo, usajili zaidi utategemea kwanza wachezaji watakaoondoka, huku Eduardo Camavinga akitajwa kuwa miongoni mwa wanaoweza kuuzwa.
Kocha wa Fulham, Álvaro Arbeloa, anafikiria kumchukua kwa mkopo chipukizi wa Real Franco Mastantuono, baada ya kuonyesha pia nia ya Gonzalo García. Lengo lake ni kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu wa 2026/27.



