Real Madrid Yamvizia Beki Lile

Klabu ya Real Madrid inaelezwa inamfatilia kwa karibu beki hodari mwenye umri  wa miaka 18 anayekipiga klabu ya Lile ya nchini Ufaransa akifahamika kama Leny Yoro.

Real Madrid inamfukuzia kwa karibu kwajili ya matumizi ya sasa na baadae kwani kijana huyo ameonesha uwezo mkubwa sana ndani ya klabu ya Lile licha ya umri wake kua mdogo, Jambo ambalo limefanya vilabu vingine kuvutiwa nae.Real MadridVinara hao wa ligi kuu nchini Hispania wamemfanya kijana huyo kua moja sajili zilizo kwenye orodha ya juu kabisa ambazo wanataka kuzifanya katika dirisha kubwa la mwezi Juni, Hii inaonesha kua sajili muhimu zitazofanyika klabuni hapo zitakua zinatoka nchini Ufaransa.

Klabu ya Real Madrid inatambua fika kua klabu zingine zinamfatilia beki Leny Yoro ikiwemo vigogo wa soka nchini Ufaransa klabu ya PSG ambayo wanaelezwa wameanza kumfanyia kazi beki huyo tangu mwezi Januari, Lakini miamba hiyo ya soka nchini Hispania wanaamini watashinda mpambano huo.Real MadridTaarifa kutoka watu wa karibu wa beki Leny Yoro zinaeleza kua kijana huyo anataka kukipiga kwa miamba ya soka kutoka nchini Hispania,Huku  akiwaeleza kabisa hata viongozi wa klabu ya Lile juu ya dhamira yake ya kukipiga ndani ya Madrid ambayo ni klabu ya ndoto zake.

Acha ujumbe