Klabu ya soka ya Real Madrid imepoteza mchezo kwa mara ya kwanza msimu huu ndani ya ligi kuu ya Hispania, Klabu hiyo imepoteza mchezo usiku wa jana dhidi ya klabu ya Rayo Vallecano.

Baada ya kupoteza mchezo huo klabu ya Real Madrid wanashuka kutoka kileleni mpaka nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kuu nchini Hispania baada ya kuvuna alama 32 kwenye michezo 13 huku Barcelona wakiongoza kwa alama 34 wakikaa juu kwa alama mbili zaidi.real madridKlabu ya Rayo Vallecano wamepindua meza mbele ya mabingwa hao watetezi baada ya kutoka nyuma kwa mabao mawili na kufunga goli la tatu liliwapa matokeo wakiwa katika dimba lao la nyumbani na kuwanyima Galacticos rekodi yao ya kuendelea bila kufungwa kwenye ligi kuu nchini Hispania.

Klabu ya Real Madrid imepata matokeo ambayo si ya kufurahisha kwenye siku za hivi karibuni baada ya wiki mbili zilizopita kupoteza rekodi ya kutokufungwa kwenye michuano yote dhidi ya Rb Leipzig, Kabla ya kupoteza jana dhidi ya Rayo Vallecano.real madridKlabu ya Rayo Vallecano ambayo ilipanda ligi kuu msimu uliomalizika imeonekana kua kiboko ya vigogo kwani msimu uliokwisha walifanikiwa kuifunga klabu ya Fc Barcelona nyumbani na ugenini kwenye ligi hiyo.

AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa