Beki wa kushoto wa Real Madrid, Ferland Mendy, amekumbwa na pigo lingine la jeraha baada ya kupata tatizo la paja ambalo linatarajiwa kumuweka nje ya uwanja kwa miezi kadhaa. Taarifa hizo zimetolewa kufuatia vipimo vilivyofanywa na klabu hiyo siku ya Jumatatu.
Mendy alipata jeraha hilo mapema katika mchezo wa La Liga dhidi ya Espanyol uliomalizika kwa ushindi wa mabao 2-0 kwa Real Madrid, ambapo alilazimika kutolewa nje dakika ya 14 pekee. Ushindi huo uliichelewesha FC Barcelona kutwaa ubingwa wa La Liga.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kupitia taarifa rasmi, klabu hiyo ilieleza “Baada ya vipimo kufanywa kwa mchezaji wetu Ferland Mendy, amebainika kuwa na jeraha la kano ya misuli ya rectus femoris katika mguu wa kulia.” Taarifa hiyo imeongeza kuwa mchezaji huyo anatarajiwa kufanyiwa upasuaji ndani ya muda mfupi.
Jeraha hilo linaongeza rekodi ya matatizo ya kiafya kwa Mendy tangu alipojiunga na Real Madrid mwaka 2019 akitokea Olympique Lyonnais, ambapo sasa ameshapata majeraha 16 tofauti katika kipindi hicho.
Chanzo kimoja cha karibu na klabu kilieleza “Ni pigo kubwa kwa Mendy na timu kwa ujumla, kwani alikuwa anaanza kurejea katika kiwango chake baada ya vipindi vya majeraha ya mara kwa mara.”
Kutokana na hali hiyo, nafasi ya Mendy kurejea katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa inaonekana kuwa ndogo, hasa kuelekea maandalizi ya Kombe la Dunia chini ya kocha Didier Deschamps.


