Klabu ya Real Madrid imethibitisha kuwachukulia hatua za kinidhamu mastaa wake Federico Valverde na Aurelien Tchouameni baada ya kuhusika katika tukio kubwa la ugomvi lililotokea wakati wa mazoezi ya timu hiyo wiki hii.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu hiyo, wachezaji hao wawili walifikishwa mbele ya mpelelezi aliyeteuliwa kufuatilia sakata hilo na kuonyesha majuto makubwa kuhusu kilichotokea. Real Madrid imewaadhibu kwa kuwatoza faini ya euro 500,000 kila mmoja ikiwa ni sehemu ya kufunga rasmi uchunguzi wa ndani wa tukio hilo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Taarifa ya klabu hiyo ilisomeka “Wachezaji wote wawili walieleza majuto yao kamili kwa yaliyotokea na wakaomba radhi kwa kila mmoja wao. Pia waliiomba radhi klabu, wachezaji wenzao, benchi la ufundi pamoja na mashabiki wa Real Madrid.”
Ripoti zinaeleza kuwa tukio hilo lilikuwa kubwa kiasi cha kumpeleka Valverde hospitalini baada ya kupata majeraha ya kichwani. Hata hivyo, Real Madrid ilithibitisha kuwa kiungo huyo kwa sasa yupo nyumbani na anaendelea vizuri huku akitarajiwa kupumzika kwa siku kati ya 10 hadi 14.
Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Valverde aliomba radhi kwa mashabiki na viongozi wa klabu, lakini akasisitiza kuwa hali hiyo haikuwa mapigano makubwa kama ilivyoripotiwa. “Kulikuwa na mabishano na kwa bahati mbaya nikagonga meza ambayo ilisababisha vurugu zaidi,” alisema kiungo huyo wa Uruguay.
Tukio hilo limeelezwa kuongeza presha ndani ya kikosi cha Real Madrid baada ya pia kuripotiwa kuwepo kwa sintofahamu nyingine iliyomhusisha beki Alvaro Carreras mapema wiki hii. Viongozi wa juu wa klabu walilazimika kufanya kikao cha dharura huku hali ya taharuki ikitajwa kuendelea ndani ya timu hiyo.


