Klabu ya Real Madrid inamuangalia kwa karibu beki wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Uingereza Reece James kama mrithi sahihi wa beki wa kulia wa klabu hiyo Dani Carvajal.

Reece James amekua na kiwango bora sana tangu apewe nafasi kwa mara ya kwanza kwenye timu ya wakubwa ya Chelsea, Licha ya majeraha ambayo yamekua yakimuandama lakini Real Madrid wanaona ndio mbadala sahihi wa Carvajal.reece jamesDani Carvajal amekua na misimu bora sana ndani ya klabu ya Real Madrid akiitumikia klabu hiyo kwa takribani misimu kumi sasa, Hivo mabingwa hao wa muda wote barani ulaya wanajhitaji mtu sahihi wa kuvaa viatu vyake.

Beki ambaye anafatiliwa kwa karibu na anaonekana anaweza kuvaa viatu vya Dani Carvajal ni beki huyo raia wa kimataifa wa Uingereza ambaye uwezo wake umedhihirika kutokana na kile ambacho anakionesha uwanjani.reece jamesReal Madrid wanaamini kama watafanikiwa kupata saini ya Reece James watakua wameziba pengo la beki Dani Carvajal kupitia mtu sahihi sana, Lakini kazi ya kupata saini ya mchezaji huyo pia sio rahisi kwani beki huyo ndio nahodha wa Chelsea lakini pia bado ana mkataba na matajiri hao wa London.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa