Riquelme Atikisa Uchaguzi wa Real Madrid Kuwasajili Haaland na Rodri

 Mgombea urais wa Real Madrid, Enrique Riquelme, amezua gumzo kubwa nchini Hispania baada ya kujitokeza kwenye kipindi cha El Hormiguero akiwa amevaa jezi ya klabu hiyo yenye jina la Erling Haaland na namba 9, hatua iliyotafsiriwa kama ujumbe wa moja kwa moja wa kampeni yake.

Riquelme Atikisa Uchaguzi wa Real Madrid Kuwasajili Haaland na Rodri

Riquelme ameahidi kufanya mageuzi makubwa endapo atamshinda mpinzani wake mkuu, Florentino Pérez, katika uchaguzi wa urais wa klabu hiyo, akiahidi kuwaleta mastaa wakubwa wa Ulaya kama sehemu ya mradi wake mpya.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Katika moja ya kauli zake kali zaidi, Riquelme alisema “Nitaweka kila juhudi kumsajili Erling Haaland na Rodri kama nitashinda urais wa Real Madrid,” akimaanisha pia kiungo wa Rodri anayeichezea Manchester City.

Riquelme Atikisa Uchaguzi wa Real Madrid Kuwasajili Haaland na RodriZaidi ya hayo, Riquelme amesaini hati ya kisheria (notary) akiahidi kuwa “Kama nitashinda urais na nikishindwa kuwaleta Haaland na Rodri, nitawalipia ada ya uanachama mashabiki wote 100,000 wa Real Madrid msimu ujao,” kauli ambayo imeibua mjadala mkubwa kutokana na gharama yake inayokadiriwa kufikia zaidi ya Euro milioni 12 (takribani Shilingi bilioni 36.6).

Riquelme Atikisa Uchaguzi wa Real Madrid Kuwasajili Haaland na RodriUchaguzi wa urais wa Real Madrid unatarajiwa kufanyika Jumapili, Juni 7, 2026, huku mashabiki na wachambuzi wakisema kinyang’anyiro hicho sasa kimepata sura ya kihistoria kutokana na ahadi kubwa na mikakati ya wagombea wote.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.