Kiungo wa Manchester City, Rodri, anatajwa kuwa tayari kushinikiza uhamisho kwenda Real Madrid iwapo mabingwa hao wa Hispania wataamua kuwasilisha ofa rasmi. Vyanzo mbalimbali vinaeleza kuwa nyota huyo wa kimataifa wa Hispania ana hamu ya kurejea La Liga, huku Manchester City ikifahamu kuwa suala la mustakabali wake linaweza kuwa gumzo kubwa msimu huu wa usajili.
Inaelezwa kuwa viongozi wa Real Madrid wamekuwa wakimfuatilia Rodri kwa muda mrefu, ingawa rais wa klabu hiyo, Florentino Perez, alikuwa bado hajaridhishwa kikamilifu na mpango wa kumsajili. Hata hivyo, kiwango bora alichoonyesha Rodri kwenye michuano ya Dunia, ambapo aling’ara na kusaidia Hispania kutwaa ubingwa, kinadaiwa kubadili mtazamo wa baadhi ya viongozi wa klabu hiyo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kwa sasa Real Madrid bado haijafanya mawasiliano rasmi na Manchester City, lakini taarifa zinaonyesha kuwa mazingira yanaendelea kufuatiliwa kwa karibu. Tayari City wameanza kuandaa mbadala iwapo Rodri ataondoka, huku majina ya Enzo Fernandez wa Chelsea na kijana Ayyoub Bouaddi wa Lille yakitajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wanaochunguzwa kuziba pengo lake.
Hispania ilipotwaa taji la Dunia, Rodri pia alitunukiwa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashindano, jambo lililozidi kuimarisha hadhi yake kama mmoja wa viungo bora zaidi duniani na kuongeza hamasa ya vilabu vikubwa kumuwania.
“Rodri tayari anafahamu masharti ya mkataba mpya ambayo Manchester City wameweka mezani, lakini hadi sasa hajaonyesha dalili za kukubali kuongeza mkataba. Kiungo huyo, ambaye sasa ameingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake, anasubiri kuona kama Real Madrid watawasiliana rasmi kabla ya kufanya uamuzi kuhusu mustakabali wake.”


