Kocha wa klabu ya Atletico Madrid raia wa kimataifa wa Argentina Diego Simeone ameongeza mkataba wa muda mrefu wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo mpaka mwaka 2027.

Kocha Simeone ambaye amedumu kwa takribani miaka 12 ndani ya klabu ya Atletico Madrid amekubali kusaini mkataba mpya ambao utamuweka kwenye viunga vya Wanda Metropolitano mpaka mwaka 2027.simeoneKocha huyo amedumu ndani ya klabu hiyo kwa muda mrefu zaidi sasa huku akiwapa mafanikio makubwa na kupata heshima kubwa mbele ya mashabiki wa klabu hiyo amekubali kuendelea kusalia klabuni hapo.

Kocha huyo raia wa kimataifa wa Argentina amekubaliana na klabu hiyo kusaini mkataba huo mpya, Huku mshahara pia ukitarajiwa kuongezeka ikumbukwe kua kocha ndie alikua kocha anaelipwa zaidi duniani.simeoneKocha Diego Simeone ameendelea kua kocha anayepewa heshima kubwa ndani ya klabu hiyo, Kwani amefanikiwa kutwaa mataji mawili ya La liga mbele ya utawala mgumu wa Barcelona na Real Madrid vilevile akifanikiwa kuifikisha fainali ya ligi ya mabingwa ulaya mara mbili klabu hiyo.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa