Kocha mkuu wa Atletico Madrid Diego Simeone na Jan Oblak waliachwa wakiomboleza kwa kipigo walichokipata jana cha bao 1-0 dhidi ya Barcelona na kulaumu kuanza kwao taratibu ndio chanzo.
Bao la Ousmane Dembele katikati ya kipindi cha kwanza lilitosha kusuluhisha mambo, huku Atletico wakishindwa kuokoa sare licha ya kutumia shinikizo la dakika za mwisho kwenye Civitas Metropolitano, ambapo Stefan Savic na Ferran Torres walipewa kadi nyekundu kwa pambano la nje ya mpira dakika za majeruhi.
Matokeo hayo yanawafanya vijana wa Simeone washindwe kuingia kifua mbele katika kinyang’anyiro cha kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa, na kocha huyo wa Atletico alikiri kwamba ufunguzi wa kusitasita kwenye mchezo huo uliigharimu timu yake.
Simeone amesema; “Ni kuanza polepole ilionekana wazi kuwa katika dakika 20 za kwanza, sio kwa sababu walitengeneza hali ya kufunga, lakini hatukuweza kutoka. Hatuweza kudhibiti kutokana na kurejesha mpira kuanza kushambulia. Baada ya bao, tulianza kuonyesha zaidi kile tunachotaka. Baada ya hapo, mechi nzuri ilichezwa, ambayo inanisisimua na kuweka mambo wazi.”
Kipa wa timu hiyo Oblak, ambaye alisimama kwa busara kumnyima Pedri kufanya matokeo kuwa 2-0 muda mfupi baada ya bao la kwanza, alikuwa na maoni sawa na kocha wake kwenye mchezo huo.
Oblak amesema kuwa; “Tulicheza mchezo mzuri isipokuwa dakika 25 za kwanza. Tulicheza vizuri sana, tulipata nafasi, lakini tulikosa bahati ya kufunga. Nadhani kwa ujumla tulicheza mchezo mzuri na tulipaswa kufunga, lakini hatukuweza kuuweka kambani.”
Baada ya Barcelona kufunga ilikuwa ngumu, lakini tulifanya kila tuwezalo. Alimaliza hivyo.