Tchouameni: Ukiwa Real Madrid ndo Utagundua Ukubwa Wake

Kiungo wa kimataifa wa Ufaransa na kalabu ya Real Madrid Aurelien Tchouameni amesema kua unaweza kujua klabu hiyo ni kubwa, Lakini utakapokua ndani yake ndo utajua ukubwa halisi.

Tchouameni ambaye alijiunga na klabu hiyo mwaka 2022 akitokea klabu ya As Monaco amesema kila mtu aanatambua ukubwa wa Real Madrid, Lakini pindi utakapojiunga na timu hiyo ndio utaona picha halisi ya klabu hiyo.TchouameniKiungo huyo anasema baada ya kujiunga na mabingwa hao mara nyingi wa ulaya ndio ameona na kuhisi ukubwa halisi wa klabu hiyo tofauti na alivyokua nje ya klabu hiyo.

Tchouameni amekua kwenye kiwango kizuri msimu huu ambapo ni msimu wake wa pili ndani ya klabu hiyo, Huku msimu uliomalizika ukiwa wa kupanda na kushuka kwake kutokana na majeraha ambayo yalikua yakimuandama.TchouameniMchezaji huyo mpaka sasa ndani ya msimu Real Madrid haijafanikiwa kupoteza mchezo wowote kiungo huyo akiwa ameanza mchezo, Hii inatoa picha ni namna gani kiungo huyo amekua muhimu na kiwango bora ndani ya klabu hiyo.

Acha ujumbe