Tebas Aomba Radhi Kwa Alichokisema Vini Kutokana na Kufanyiwa Ubaguzi wa Rangi

Rais wa LaLiga Javier Tebas ameomba radhi kwa kupendekeza Vinicius Jr alikuwa “alidanganya” wakati winga huyo wa Real Madrid alipokemea ubaguzi wa rangi aliofanyiwa nchini Uhispania.

 

Tebas Aomba Radhi Kwa Alichokisema Vini Kutokana na Kufanyiwa Ubaguzi wa Rangi

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil alitumia mtandao wa kijamii kuzungumza baada ya kunyanyaswa katika mechi ya Jumapili huko Valencia, akisema ni tatizo ambalo amevumilia katika muda wote wa ligi.

Jibu la Tebas kwenye Twitter alisema “Kabla ya kuikosoa na kuitusi LaLiga, unahitaji kujijulisha vizuri, Vini Jr. Usikubali kudanganywa”, yalikosolewa vikali kwa kutolishughulikia suala hilo na bosi huyo wa LaLiga amelishughulikia sasa akiomba radhi.

Tebas amesema; “Nadhani ujumbe, na nia niliyokuwa nayo, haikueleweka na idadi kubwa ya watu, haswa huko Brazil. Sikutaka kumshambulia Vinicius, lakini ikiwa watu wengi walielewa hivyo, ninahitaji kuomba msamaha. Haikuwa nia yangu, nilijieleza vibaya, kwa wakati mbaya.”

Tebas Aomba Radhi Kwa Alichokisema Vini Kutokana na Kufanyiwa Ubaguzi wa Rangi

Tebas, katika kutetea mtazamo wa ligi haswa kuhusiana na Vinicius aliongeza kuwa ikiwa ataumiza mtu na kudhani yeye ni mbaguzi wa rangi ni mbali na ukweli hivyo anasikitika kwa kile kilichotokea na ndiyo maana walishutumu.

“Tulizungumza na vilabu, ili waweze kutoa usalama zaidi, watambue mashabiki. LaLiga inamtunza Vinicius. Na ikiwa hawakuelewa kilichotokea lazima niombe msamaha.”

Vinicius alitishia kuondoka uwanjani katika kipindi cha pili cha Mestalla baada ya kuimbwa na nyimbo zinazodaiwa kuwa za ubaguzi na Real na aliwasilisha malalamiko katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Uhispania.

Tebas Aomba Radhi Kwa Alichokisema Vini Kutokana na Kufanyiwa Ubaguzi wa Rangi

Valencia walipewa adhabu ya kutocheza mechi tano na mashabiki na kutozwa faini ya euro 45,000 (pauni 39,000) – adhabu ambayo klabu hiyo iliiita isiyo na uwiano kabisa walipothibitisha kuwa watakata rufaa, huku kocha mkuu Ruben Baraja akiapa kupambana na machafuko hayo .

Kocha wa Uingereza Gareth Southgate ameongoza wito wa kupewa adhabu kali tangu timu yake ilipokaribia kuondoka uwanjani baada ya wachezaji kufanyiwa ubaguzi wakati wa mechi iliyofanyika Bulgaria mwaka 2019.

Southgate amesema; “Ni hali ya kuchukiza. Nadhani ni mbaya sana kwamba inaonekana kama italazimisha mabadiliko. Natumai kutakuwa na kitu chanya kutoka kwao”

Tebas Aomba Radhi Kwa Alichokisema Vini Kutokana na Kufanyiwa Ubaguzi wa Rangi

Vinicius, ambaye kadi yake nyekundu dhidi ya Valencia Jumapili ilifutiliwa mbali, alikosa mchezo wa Real wakiwa nyumbani dhidi ya Rayo Vallecano kwa malalamiko madogo ya goti lakini alikuwa uwanjani kuwaona wachezaji wenzake wakivalia jezi zenye namba na jina lake mgongoni kabla ya mchezo kuanza .

Acha ujumbe