Golikipa wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Ujerumani Marc Andre Ter Stegen amefanikiwa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu ya Barcelona mpaka mwaka 2028.
Golikipa huyo ambaye amaitumikia klabu hiyo kwa muda mrefu amekubali kusaini kandarasi mpya ambayo itaendelea kumuweka ndani ya viunga vya Camp Nou mpaka mwaka 2028 licha ya tetesi za yeye kuondoka klabuni hapo kwa muda kidogo.Klabu ya Barcelona kupitia rais wake Joan Laporta ilieleza mapema kua moja ya wachezaji ambao hawagusiki ndani ya klabu hiyo basi ni golikipa Ter Stegen na wamefanikiwa kuendelea kumbakiza klabuni hapo kw amuda zaidi.
Klabu ya Barcelona baada ya kumsainisha golikpa huyo mkataba mpya pia wameweka kiwango kikubwa cha pesa ambacho ni Euro milioni 500 kwa klabu yeyote ambayo itahitaji huduma ya golikipa huyo raia wa kimataifa wa Ujerumani.Golikipa Ter Stegen amekua kwa muda mrefu ndani ya timu akicheza kwa mafanikio makubwa na mpaka sasa anakua nchezaji aliyedumu kwa muda mrefu klabuni hapo kando ya Sergio Roberto kwa wachezaji ambao wapo klabuni mpaka sasa.