Toni Kroos Aiponda Ligi ya Saudia

Kiungo wa klabu ya Real Madrid na mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani Toni Kroos ameiponda ligi kuu ya soka ya Saudia Arabia maarufu kama Saudian Pro League.

Toni Kroos ameonesha kutokufurahishwa na kinachoendelea kwasasa kwa wachezaji wengi wa soka kuondoka barani ulaya na kutimkia nchini Saudia Arabia jambo ambalo kiungo huyo haonekani kuliunga mkono.Toni KroosKiungo huyo anaeleza kua inaelezwa kua ni mpira wa hamasa unaochezwa Saudia lakini kila kitu kipo kwajili ya pesa kule, Hivo ni wazi imekua pesa dhidi ya mpira wa miguu mpaka sasa.

Mchezaji huyo alionesha wazi kukerwa na ambayo yanaendelea nchini Saudia wiki moja nyuma juu uhamisho wa kiungo Gabriel Viega, Lakini amefanya mahojiano tena na kusema Saudia inapmbana dhidi ya mpira halisi kwa kutumia pesa.Toni KroosVilabu mbalimbali kutoka nchini Saudia Arabia vimeonekana kutumia pesa nyingi sana kusajili wachezaji kutoka barani ulaya na hii ndio inatafsiriwa na kiungo Toni Kroos kua wametumia ushawishi mkubwa wa pesa kuliko mapenzi halisi ya mpira wa miguu.

Acha ujumbe