Kiungo wa klabu ya Real Madrid raia wa kimataifa wa Uruguay Federico Valverde amezungumza na kusema hajioni akiwa nje ya klabu hiyo mabingwa watetezi wa ligi ya mabingwa barani ulaya.

Valverde wakati akifanya mahojiano na chombo kimoja cha habari jijini Madrid amesema kua kwasasa kuondoka kwake ndani ya Real Madrid labda klabu hiyo imuue, Kupitia kauli hiyo imeweka wazi kua hana mpango wa kuondoka ndani ya klabu ya Real Madrid siku za usoni.ValverdeKiungo huyo wa kimataifa wa Uruguay amekua moja ya wachezaji muhimu ndani ya kikosi cha Real Madrid chini ya kocha Ancelotti, Lakini imeripotiwa vilabu mbalimbali  kutoka ligi kuu ya Uingereza vimekua vikimnyemelea mchezaji huyo ili waweze kupata huduma yake.

Federico Valverde ambaye ametoka kwenye akademi ya klabu ya Real Madrid na kupandishwa timu ya wakubwa, Ameonesha kiwango kikubwa tangu alipopata nafasi kwenye timu ya kwanza huku akiwa moja ya mchezaji mwenye mchango mkubwa kwenye taji la ulaya msimu uliomalizika.ValverdeReal Madrid wenyewe kama klabu inaripotiwa haipo kwenye mpango wowote wa kumuuza Valverde kwakua wanamuona kama mchezaji ambae anaweza kuendeleza mradi wao baada ya viungo wakongwe klabuni hapo kama Modric, na Kroos kustaafu hivo wababe hao hawana mpango wa kumuachia kiungo huyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa