Villarreal Yampa Mkataba Mpya Parejo

Klabu ya Villarreal imefanikiwa kumpa mkataba mpya kiungo wake mkongwe Dani Parejo ambaye ataendelea kuwepo kwenye viunga vya Estadio de la ceramica mwaka 2026.

Kiungo huyo ambaye ana miaka minne klabuni hapo ambapo alijiunga na Villarreal mwaka 2020 ambapo ameitumikia klabu hiyo mpaka sasa, Ambapo amekubali kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuwatumikia nyambizi hao wa njano.villarrealDani Parejo amekua na kiwnago bora tangu ajiunge na klabu hiyo mwaka 2020 ambapo alionekana kama ubora wake umeisha na klabu yake ya zamani ya Valencia ambayo aliitumikia kwa takribani miaka kumi lakini tangu ajiunge na nyambizi wa njano ameendelea kutakata.

Kiungo huyo wa zamani wa vilabu vya Real Madrid na Getafe amekua kwenye na mwendelezo bora wa kiwango tangu akiitumikia klabu ya Valencia na sasa klabu yake ya Villarreal jambo ambalo lilimfanya kudumu Valencia kwa takribani miaka 10 na sasa ndani ya nyambizi wa njano akiwa na miaka minne na sasa ameongeza mingine miwili ambapo akimaliza atakua na jumla ya miaka sita.

Acha ujumbe