Winga wa klabu ya Real Madrid Vinicius Jr ameripotiwa kutimka kwenye kambi ya timu ya taifa ya Brazil baada ya kuripotiwa kupata majeraha ya misuli ya paja mapema leo.
Vinicius Jr ambaye alikua kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kilichopokea kichapo cha mabao mawili kwa moja dhidi ya Colombia, Huku akiwa amesaidia upatikanaji wa goli moja la Brazil kwa kupiga pasi ya bao kwa Gabriel Martinelli.Winga huyo ameripotiwa anajiandaa kurejea jijini Madrid kwajili ya kwenda kufanyiwa uchunguzi zaidi na jopo la madaktari wa klabu yake ya Real Madrid ili kugundua ukubwa wa jeraha ambalo amelipata mchezaji huyo.
Vyanzo vya ndani vinaeleza kua jeraha la sasa alilolipata mchezaji huyo sio kubwa kama ambalo alilipata awali mwanzoni wa msimu huu na kumuweka nje ya uwanja kwa wiki kadhaa.Taarifa rasmi juu ya ukubwa wa jeraha la Vinicius Jr utatolewa baada ya mchezaji huyo kufika nchini Hispania na kufanyiwa vipimo na madaktari klabuni hapo, Licha ya kuelezwa jeraha lake sio kubwa kama lililompata awali.