Winga wa klabu ya Real Madrid raia wa kimataifa wa Brazil Vinicius Jr na kiungo Arda Guler wametajwa kurejea katika kikosi hicho baada ya kua nje ya uwanja kwa majeraha.
Vinicius Jr alipata majeraha takribani mwezi mmoja na nusu huku kiungo Arda Guler amekua akipata majeraha na kupona mara kwa mara, Huku akiwa hajafanikiwa kucheza mchezo wowote ndani ya klabu hiyo tangu ajiunge dirisha kubwa lililopita.Katika kuthibitisha hilo kocha wa klabu hiyo Carlo Ancelotti ameeleza wachezaji wake wawili wamerejea uwanjani, Hivo ni wazi watarejea katika michezo ya mbeleni ambayo klabu hiyo itakua inacheza.
Kurejea kwa wachezaji hao wawili ni wazi ni faida kwa klabu ya Real Madrid katika kuimarisha kikosi chao, Kwani kwa mchezaji kama Vinicius Jr amekua mchezaji muhimu sana ndani ya kikosi cha Real Madrid hivo kurejea kwake ni jambo kubwa ndani ya timu hiyo.Mchezaji Arda Guler na yeye kwa upande wake inaelezwa inawezekana anaweza kucheza mchezo wake wa kwanza kesho tangu ajiunge ndani ya klabu hiyo ambapo Real Madrid watakua nyumbani kuikaribisha klabu ya Real Mallorca.