Winga wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil Vinicius Jr ametangazwa kama kiongozi wa kampeni ambayo imeanzishwa ili kupingana na masuala ya ubaguzi wa rangi.
Shirikisho la soka la mpira wa miguu duniani FIFA limeanzisha kampeni ya kupingana na ubaguzi wa rangi ambao umekua ukiendelea na Vinicius Jr ameteuliwa kua kiongozi wa kampeni hiyo kwani hivi karibuni mchezaji huyo amekua akikumbana na na vitendo vya ubaguzi mara kwa mara.Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Gianni Infantino amesema amemchagua winga huyo wa Real Madrid kua kiongozi wa kampeni hiyo pamoja na baadhi ya wachezaji wengine, Huku akiwaagiza kuja na pendekezo la sheria kali dhidi ya wabaguzi ambazo zitafatwa na mashirikisho yote ya mpira duniani.
Vinicius Jr atapata fursa ya kupendekeza sheria zitakazowaadhibu watu wanaoeleta vitendo vya ubaguzi kwenye mpira wa miguu kuanzia kwa wachezaji mpaka mashabiki, Kupitia hii inaweza hatua nzuri ya kuweza kutokomeza ubaguzi uwanjani.Winga Vinicius Jr amekua akikumbana sana na vitengo vya ubaguzi sana ndani ya ligi kuu ya Hispania haswa kwenye viwanja vya ugenini ambavyo amekua akicheza, Kutokana na kua kampeni hii iliyoanzishwa kwa inaweza kuleta majibu ya nini kifanyike ili kutokomeza ubaguzi wa rangi michezoni.