Kocha wa klabu ya Fc Barcelona Xavi Hernandez amesema hajazingatia uchambuzi unaofanywa baada ya wao kutolewa michuano ya Europa kwakua hautabadilisha chochote.

Kocha Xavi kwasasa amesema nguvu yote anaihamishia katika ligi kuu ya Hispania msimu huu La liga baada ya kutolewa kwenye michuano ya kombe la Europa katikati ya wiki hii na klabu ya Manchester United mchezo uliopigwa katika dimba la Old Trafford na Bracelona kufungwa ambao mawili kwa moja.xaviKocha huyo anasema hawatasikiliza wanaowakosoa zaidi wao wanasonga ambapo alieleza katika mchezo dhidi ya Man United walicheza vizuri na ilionekana Barcelona yenye taswira nzuri, Hivo ni matokeo tu hayakua upande wao lakini nguvu zote wanahamishia kwenye kombe la ligi kuu ya Hispania kwasasa.

Barcelona watashuka dimbani siku ya Jumapili kumenyana na klabu ya Almeria huku wakiwa ugenini na kocha Xavi anasema mchezo huu sasa hivi ndio mchezo muhimu zaidi kwao kuliko kuangalia michezo ambayo tayari imeshapita. xavi Barcelona chini ya kocha Xavi wameonesha umahiri mkubwa haswa kwenye ligi kuu ya Hispania ambayo mpaka sasa wanaongoza kwa alama nane juu ya mabingwa watetezi klabu ya Real Madrid ambao wanashika nafasi ya pili, Lakini Barcelona wameonekana kutokufanya vizuri msimu huu kwenye michuano ya ulaya.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa