Xavi Kuongezewa Mkataba Barca

Mkurugenzi wa klabu ya Barcelona Deco amesema wapo kwenye mchakato wa kumuongezea mkataba mpya kocha wa klabu hiyo Xavi Hernandez ambaye alijiunga na timu hiyo mwaka 2021.

Deco anasema kocha Xavi amefanya kazi nzuri tangu ajiunge na klabu ya Barcelona hivo anastahili kupewa mkataba mpya, Huku akigoma kuweka wazi kua ataongezewa mkataba wa muda gani ndani ya timu hiyo.xaviKocha huyo ambaye amejiunga na klabu hiyo mwaka 2021 akitokea Al Sadd ya nchini Qatar amefanikiwa kwa kiwango fulani ndani ya klabu ya Barcelona na ndio sababu ya Deco kuona kocha huyo anastahili kuongezewa mkataba.

Mkurugenzi Deco amesema wanaamini kocha huyo ambaye pia ni gwiji wa zamani wa klabu hiyo anaweza kuiboresha klabu hiyo kwakua wanaamini katika mipango ya mbele na mtu sahihi ni kiungo huyo wa zamani wa klabu hiyo.xaviKocha Xavi ameshafanikiwa kutwaa ubingwa ligi kuu ya Hispania kwenye msimu wake wa pili ndani ya Barcelona na kombe la Spanish super cup, Huku akiwa ameshindwa kufurukuta tu kwenye michuano ya ulaya lakini Barcelona wanaamini klabu hiyo iko mikono salama chini ya kocha huyo.

Acha ujumbe