Kocha wa klabu ya Barcelona Xavi Hernandez amebainisha kua hakuna matatizo ndani vyumba vya kubadilishia nguo ndani ya klabu hiyo kutokana na kauli aliyoitoa kiungo Gundogan.
Kiungo Ilkay Gundogan jumamosi iliyomalizika alitoa kauli ambazo zilionekana kama zinawashambulia wachezaji wenzake, Lakini kocha Xavi amekanusha jambo hilo na kusema kila kitu kipo sawa.Kocha huyo amesema kua kitu ambacho alikilenga Gundogan ni kutaka kuwakumbusha wachezaji wenzake jambo, Lakini wako pamoja kama timu na alichokionesha Gundogan ni kua na uchu wa ushindi.
Kocha huyo alisistiza zaidi kua kama timu wako pamoja na hakuna matatizo yoyote yanayoendelea ndani ya timu yao kama ambavyo taarifa zilikua zinaeleza huenda kauli ya Gundogan ikaharibu mahusiano yake na wachezaji wenzake.Aidha kocha Xavi ameweka wazi kurejea kwa kiungo wako ambaye amekosekana uwanjani kwa wiki kadhaa Pedri, Amesema mchezaji huyo yupo fiti aslimia 100 kurejea kukipiga uwanjani.