Kocha wa klabu ya Barcelona Xavi Hernandez ameweka wazi kua klabu hiyo haina mpango wa kusajili mchezaji yeyote katika dirisha dogo la mwezi Januari licha ya majeraha ambayo wamekua wakiyapata.
Xavi ameweka wazi kua kiuhalisia hawataingia sokoni katika dirisha hili dogo licha ya kwamba anaona katika dirisha hili walipaswa angalau kuongeza wachezaji, Lakini uhalisia ni kua hawataweza kusajili mchezaji mwingine.Kocha huyo anaamini baada ya majeraha ambayo aliyapata kiungo wake Pedri walipaswa kuingia sokoni kwajili ya kuboresha kikosi chao, Lakini pia ameeleza kua wanaweza kuangalia uwezekano wa kufanya hivo japo uhalisia utabaki palepale kua ni ngumu wao kusajili Januari hii.
Klabu ya Barcelona imekua ikiandamwa na majeraha haswa kwa wachezaji wake wa kikosi cha kwanza kama Gavi, na Pedri lakini hawatweza kuingia sokoni katika dirisha dogo la Januari kutokana na hali ya kiuchumi ya klabu hiyo.Kutokana na matatizo ya kiuchumi ambayo yanaikabili klabu ya Barcelona ndio sababu kocha Xavi ameona ni vigumu kwao kuingia sokoni katika dirisha hili dogo na kuongeza mchezaji mwingine licha ya majeraha ambayo yamekua yakiwandama.