Xavi Ashtushwa na Taarifa za Alves

Kocha wa klabu ya Barcelona Xavi Hernandez ameshtushwa na taarifa za mchezaji mwezake wa klabu ya Barcelona Davi Alves ambaye anatuhimiwa kuhusika na unyanyasaji wa kingono.

Beki wa kimataifa wa Brazil Dani Alves mwenye umri wa miaka 39 alikamatwa jana jijini Barcelona kutokana na kutuhumiwa kufanya unyanyasaji wa kingono, Taarifa hiyo imepelekea kocha Xavi kushtushwa na taarifa kuhusu gwiji Dani Alves.xaviKocha Xavi ambaye alimsajili beki huyo kwa mkataba wa muda mfupi ndani ya klabu ya Fc Barcelona, Kocha huyo amesema taarifa hiyo imemshtusha sana ameyazungumza hayo kwenye mahojiano na waaandishi wa habari siku ya leo kuelekea mchezo wa ligi kuu nchini Hispania dhidi ya Getafe.

Kocha huyo amewaambia wanahabari kua suala hilo ni suala la kisheria hivo sheria ndio itaamua chochote juu ya tuhuma hizo, Lakini yeye aliishia kushtushwa na taarifa hizo juu ya mchezaji mwenzake huyo wa zamani ndani ya klabu ya Barcelona.xaviDani Alves ambaye aliweka rekodi ya mchezaji mkubwa zaidi wa Brazil kushiriki michuano ya kombe la dunia nchini Qatar 2022 alikamatwa na polisi jijini Barcelona akituhumiwa na vitendo vya unyanyasaji wa kingono, Huku taarifa zaidi zikiwa zinasubiriwa kutoka kwenye mamlaka nchini Hispania.

Acha ujumbe