Kocha wa klabu ya Fc Barcelona Xavi Hernandez amefunguka kua huu ni muda wa klabu hiyo kufungua ukurasa mpya baada ya kutolewa kwenye ligi ya mabingwa barani ulaya.xaviBarcelona ambao wametolewa katika ligi ya mabingwa ulaya msimu huu kwenye hatua ya makundi na kushindwa kufika hatua ya mtoano, lakini kocha huyo anaamini ni muda wa kuanza upya na kuanza kutolea macho michuano mingine.

Licha ya kutumia gharama kubwa sokoni kwenye dirisha lililopita pamoja na kua na matatizo ya kifedha lakini haikusaidia kwa klabu ya Barcelona kufanya vizuri kwenye ligi ya mabingwa ulaya msimu.xaviKocha Xavi anaamini wanahitaji kufanya kupambana katika michuano mingine hasa ligi ya nyumbani ambapo wako nyuma kwa alama tatu nyuma ya vinara wa kigi hiyo klabu ya Real Madrid.

Kocha Xavi anaamini kufeli kwao kwenye ligi ya mabingwa msimu kutakua chachu ya wao kufanya vizuri katika michuano mingine kama kombe la liga,Copa de le rey, pamoja na Spanish super cup.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa