Sterling na Madrid; Mambo Kunoga!

Imewekwa wazi kuwa klabu ya soka ya Real Madrid inamtaka mchezaji mshambuliaji wa klabu ya soka ya Manchester City inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza chini ya bosi Pep Guardiola, Raheem Sterling mwenye umri wa miaka 23 kwa sasa.

Inasemekana kuwa klabu hiyo inayokipiga pale La Liga, Hispania ilianza kumfuatilia mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza tangu kitambo kwa mujibu wa Sky Sports. Unadhani mambo yatanoga au dili itabuma?

Acha ujumbe