Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, inatarajia kushuka dimbani hii leo saa 2 usiku kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, kuanza kampeni ya kuwania ubingwa wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) kwa kuvaana na timu ya Burkina Faso.

Mchezo huu wa Taifa Stars ni mchezo wa ufunguzi wa fainali hizo, ambazo kwa mara ya kwanza zimeandaliwa kwa ushirikiano wa nchi tatu za Afrika Mashariki, Tanzania, Kenya na Uganda. Michuano itapigwa kwenye miji minne ya ukanda huo, Dar es Salaam, Zanzibar, Nairobi na Kampala, na inahusisha jumla ya timu 19 zilizopangwa katika makundi manne.
Bingwa mtetezi wa CHAN ni Senegal, ambaye anasubiri kuona nani atakuwa tishio kwao mwaka huu.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kwa upande wa Taifa Stars, hii ni fursa adhimu si tu kuonyesha uwezo wao mbele ya mashabiki wa nyumbani, bali pia kuandika historia mpya dhidi ya timu yenye uzoefu kama Burkina Faso. Mchezo huu ni zaidi ya alama tatu ni kuhusu heshima, uzalendo na kuanza michuano kwa kishindo
Kwa kuonyesha dhamira ya kuinua hadhi ya michuano ya CHAN, CAF imeongeza zawadi ya fedha kwa bingwa hadi Dola za Kimarekani milioni 3.5, ongezeko la 75% kutoka toleo lililopita. Aidha, mfuko mzima wa zawadi sasa umefikia Dola milioni 10.4, ongezeko la 32%.


