Tetesi za Usajili

Mshambuliaji wa RB Leipzig na Ujerumani, Timo Werner, 24, yupo tayari kujiunga na Liverpool kama vinara hao wapo tayari kulipa £52m.

Kiungo wa Chelsea na Brazil, Willian, 31, yupo kwenye mazungumzo na Liverpool kumsajili iwapo mkataba wake utakapomalizika.

Borussia Dortmund wapo tayari kumfanya winga wake Jadon Sancho, 20, kuwa mchezaji pili anayelipwa pesa nyingi ili kumbakiza kwenye klabu pamoja na Manchester United na Chelsea kuonyesha nia.

Manchester United wanafikiria kumuuza beki wa Diogo Dalot, 21, kwa Paris St-Germain.

Philippe Coutinho atarejea katika ubora wake iwapo kiungo huyo ataondoka Barcelona na kujiunga na Chelsea, amesema mkongwe wa Brazil Rivaldo.

Liverpool wamemwambia Coutinho hawana lengo la kumrejesha kutoka Barcelona.

Mchezaji wa zamani wa Liverpool na Chelsea, Glen Johnson ameitaka The Blues imsaini Coutinho.

Leicester City wamejiandaa kuchuana na Manchester United kuwania saini wa straika wa Borussia Monchengladbach Alassane Pea, 27.

Manchester United waanza kumuwinda kiungo wa Aston Villa, Jack Grealish kama winga wa kulia iwapo dili hilo litakamilika.

Jack Grealish

Juventus watarajia kutuma ofa kwa straika wa Napoli ambae ni raia wa Poland Arkadiusz Milik, 26.

Kiungo wa Arsenal Muarmenian, Henrikh Mkhitaryan, 31, anamatumaini atabaki Italia akiwa na ROMA kwa msimu ujao kwa mkopo, wakati Beki wa Man United, Chris Smalling, 30, akitegemea kurefusha mkataba wake wa mkopo baada ya kufanya vizuri kwa mkopo akiwa na Inter Milan.

Arsenal wanajiandaa kumchukua jumla beki wa Flamengo Mhispania Pablo Mari, 26, ambae alijiunga kwa mkopo Januari.

Juventus wanatafuta mnunuzi wakumnunua winga wa Italia Federico Bernardeschi, 26.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.