BAADA ya kumtambulisha kiungo mshambuliaji kutoka Ghana, James Akaminko, Uongozi wa Azam FC umefunguka kuwa bado usajili wa beki kisiki ambao utakamilisha usajili wao kwenye dirisha kubwa la usajili.

Azam mpaka sasa imefanya usajili wa nyota watano wa kigeni ambao ni Kipre Junior, Ally Ahamada, Tape Edinho, Isah Ndala na Akaminko.

Azam, Beki Kufunga Usajili Azam, Meridianbet

Akizungumzia usajili wao, Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria ‘Zaka zakazi’ amesema kuwa “Akaminko ni mchezaji ambaye anaweza kucheza namba zaidi ya mbili, anaweza kucheza namba sita, nane hata 10.

“Baada ya usajili wa Akaminko pia bosi amesema kuwa atashusha beki wa kati ambaye ataongeza nguvu kwenye kikosi chetu na huo utakuwa usajili wetu wa mwisho.”

Kulingana na mipango waliyonayo Azam FC pamoja na aina ya wachezaji waliowasajili hii inaonyesha kuwa ligi ya msimu ujao itakuwa na ushindani mkubwa tofauti na misimu mingine iliyopita.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa