Klabu ya Newcastle United  wanakabiliwa na kibarua kizito cha kumbakisha kiungo wao Bruno Guimaraes kutokana na mchezaji huyo kuhitajika na vilabu vikubwa barani Ulaya ikiwemo Liverpool na Chelsea.

 

Guimaraes wa Newcastle Anawindwa na Chelsea, Madrid na Liverpool.

Bruno, ambaye ni raia wa Brazil mkataba wake ndani ya Newcastle United ni hadi 2026 na inasemekana kuwa klabu hiyo wanataka kumpa masharti ambayo yatakayokuwa bora kwake.

Lakini vyombo vya habari mbalimbali  vya Brazil vinaripoti kwamba Real Madrid, Liverpool na Chelsea wote wanamfuatilia kwa karibu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 huku dirisha dogo la usajili likiwa karibu kufunguliwa hapo Januari.

Guimaraes wa Newcastle Anawindwa na Chelsea, Madrid na Liverpool.

Guimaraes alitokea Lyon kwa uhamisho wa Pauni milioni 40 Januari iliyopita, na timu hizo za Uingereza na moja ya Uhispania wanaona kuwa usajili wa mchezaji huyo unaweza kuongeza kitu kwenye vikosi vyao.

Newcastle wanashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi kuu ya Uingereza baada ya kucheza michezo 12 huku kiungo huyo akifunga mara mbili na kutoa pasi mbili za mabao katika mechi tisa alizoanza. Real wameripotiwa kumtaka mchezaji huyo  kama mbadala wa Casemiro aliyehamia Manchester United majira ya joto.

Guimaraes wa Newcastle Anawindwa na Chelsea, Madrid na Liverpool.

Liverpool wanaendelea kutafuta viungo kwaajili ya kuongeza nguvu na Guimaraes ni chaguo lao pamoja na Jude Bellingham, wakati Chelsea wanaweza kumpoteza N’Golo Kante ambaye hawajakubaliana bado katika kuobgeza mkataba na Jorginho mwishoni mwa msimu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa