Klabu ya Real Madrid ya Uhispania wanapanga kumsajili mshambuliaji wa Tottenham Heung-Min Son mwenye umri wa miaka 30.

 

Son Ananyemelewa na Real Madrid.

Mchezaji huyo maarufu wa Korea Kusini, msimu uliopita alichukua kiatu cha Dhahabu pamoja na mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah baada ya kufungana kwenye kufunga  mabao 23 kwenye Ligi kuu ya Uingereza.

Bado hajafikia kiwango kile kile msimu huu, hata hivyo jarida la Ujerumani la Sport1 linasema Kocha wa Los Blancos Carlo Ancelotti amekuwa akimwangalia mchezaji huyo kwa jicho la tatu.

Son ana mkataba mrefu  unaomuweka klabuni hapo hadi mwishoni mwa msimu wa joto wa 2025 Kaskazini mwa London na hajawahi kuweka  hadharani nia ya kuondoka, baada ya kufurahia ushirikiano mzuri na Harry Kane katika misimu ya hivi karibuni.

Son Ananyemelewa na Real Madrid.

Lakini kukua kwake kunamaanisha kwamba wakati ni muhimu ikiwa anataka kuondoka kwenda kwenye  malisho mapya, ambayo yanaweza kuakisi hali ambayo Sadio Mane alibadilisha kutoka Liverpool na kwenda Bayern Munich miezi minne iliyopita.

Son na Tottenham walitajwa kama farasi weusi ambao wangeweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza  baada ya kuanza msimu vizuri wakiwa na kocha wao Antonio Conte, Lakini kupoteza mechi  mfululizo kumewafanya wabaki pointi tano nyuma ya wapinzani wao na vinara wa Ligi  Arsenal licha ya kuwa wamecheza mechi moja zaidi.

Huku mchezaji mwenzake Harry Kane mwenye umri wa miaka  29, akiwa anawindwa na vilabu vya Manchester City na Bayern Munich katika siku za hivi karibuni na ana uhakika wa kuvutia mashabiki zaidi mwishoni mwa kampeni ya sasa.

Son Ananyemelewa na Real Madrid.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa