Klabu ya Manchester United wanataka kumrejesha Memphis Depay Old Trafford ambaye kwasasa anatumikia klabu ya Barcelona ya huko Uhispania ambayo imekuwa ngumu kwake kucheza.

 

United Inataka Kumrudisha Memphis Depay

Memphis Depay ambaye yupo kwenye Kombe la Dunia akiwa na Uholanzi, mshambuliaji  huyo anaonekana kuwa wa ziada kwa mahitaji ya Barcelona miezi 18 tu baada ya kuwasili kutoka Lyon ya Ufaransa.

Sport ya nchini Uhispania inadai United imekuwa ikifuatilia kwa karibu hali ya Depay huko Camp Nou kwa nia ya kumsajili tena katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari baada ya aliyekuwa mchezaji wao gwiji Ronaldo kuondoka.

Depay mwenye umri wa miaka 28 alishindwa kuonyesha makali yake kipindi chake cha kwanza huko Manchester, alifunga mabao saba katika mechi 53 baada ya kujiunga kwa pauni milioni 31 kutoka PSV Eindhoven msimu wa joto wa 2015.

United Inataka Kumrudisha Memphis Depay

Mchezaji huyo aliingia akitokea benchi wakati nchi yake ilipoilaza Senegal 2-0 Jumatatu kwenye michuano ya Kombe la Dunia, aliuzwa kwa Lyon miezi 18 baadaye lakini kuondoka kwa Cristiano Ronaldo United kunamaanisha kuwa sasa kuna nafasi katika kikosi cha Erik ten Hag kwa mshambuliaji mwingine.

Lakini dili hilo bila shaka litakuwa la kuvutia kifedha, huku miamba hao wa Uhispania wakiripotiwa kuwa tayari kumwacha Depay ahamie bure ikiwa atakubali kuvunja mkataba wake uliosalia.

United Inataka Kumrudisha Memphis Depay

Ripoti hiyo hiyo pia inaangazia hamu ya Barcelona kumnunua beki wa kulia wa United Mreno Diogo Dalot, ambaye amekuwa mmoja wapo wa hadithi za mafanikio za mapema za Ten Hag Old Trafford.


Kombe la Dunia Linatimua Vumbi huko Qatar ni timu 32, sawa na mechi 64 zitapigwa kwenye viwanja tofauti. Meridianbet wana uwanja wao wa Kushiriki na wewe wakati Michuano hii inaendelea. Uwanja wa Machaguo Spesho ni Kwa ajili yako, wewe Bingwa wa Kubeti. Unaweza kubeti ni Timu gani itachukua Ubingwa, Timu gani Itaongoza kuwa na kadi nyingi za Njano na Nyekundu, au Timu gani itatoka mapema kwenye michuano hiyo. Uamuzi ni wako. Chaguo ni lako. Hii ipo mpaka mwisho wa Kombe la Dunia.

BONYEZA HAPA

 

 

United, United Inataka Kumrudisha Memphis Depay, Meridianbet

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa