Manchester United na Chelsea wameambiwa ni nini wanapaswa kulipa ili kumpata beki wa kulia wa Inter Milan na timu ya Taifa ya Uholanzi Denzel Dumfries.

 

United, United na Chelsea Waambiwa Bei ya Dumfries, Meridianbet

Dumfries ambaye ana miaka 26, kwa sasa anafanya vyema katika michuano ya Kimataifa kwa mwaka wa pili mfululizo, akiwa ameng’ara vyema kwa Uholanzi wakati wa fainali za Euro 2020 zilizocheleweshwa msimu uliopita.

Nchini Qatar, amekuwa mmoja wa wachezaji waliocheza vizuri zaidi wa Louis van Gaal na alivutia zaidi katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Marekani Jumamosi katika hatua ya 16 bora, akifunga bao moja na kutoa pasi mbili za mabao.

Ubora huo umeongeza hamu kwa vilabu vikubwa vya Ligi Kuu vikiwemo United na Chelsea, huku Arsenal na Tottenham pia zikifikiria kumpata mchezaji huyo dirisha dogo la Januari.

United na Chelsea Waambiwa Bei ya Dumfries

Ripoti kutoka nchini Italia zinasema kuwa ni Blues na United ndio  wanaoongoza kundi la wanaomuwinda mchezaji huyo huku Calciomercato wakidai kwamba ofa ya pauni milioni 43 pamoja na nyongeza ya pauni milioni 8.6 itakuwa vigumu kwa Inter kukataa, iwe Januari au msimu ujao wa joto.

Ingawa Dumfries mwenyewe hana haraka ya kuondoka Italia, anasemekana kufurahia matarajio ya kucheza Uingereza siku za usoni na kuna uwezekano mkubwa wa makubaliano kufikiwa mwishoni mwa kampeni lakini kwasababu ya hali mbaya ya kifedha ya Inter, hawataweza kukataa pesa nyingi mwezi ujao.

United na Chelsea Waambiwa Bei ya Dumfries

Kwa hivyo itategemea ni kiasi gani United na Chelsea wanatamani kumpata mchezaji wao. Dumfries na wenzake wa Uholanzi watamenyana na Argentina katika robo fainali ya Kombe la Dunia Ijumaa jioni.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa