Nyota wa Morocco na timu ya Chelsea Hakim Ziyech amekataa kuondoka Chelsea mwezi Januari huku AC Milan ikionyesha nia ya kumtaka kumsajili mchezaji huyo.

Winga huyo alijiunga na The Blues kwa pauni milioni 33.3 mwaka 2020 lakini amekuwa na wakati mgumu kwa kushindwa kuonyesha kiwango kizuri mara kwa mara alipokuwa Stamford Bridge chini ya kocha Thomas Tuchel.
Akiwa ameanza mara moja tu katika Ligi kuu ya Uingereza msimu huu, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amekiri kwamba huenda atalazimika kutafuta malisho mapya kutokana na kutopata nafasi kwa Potter.

Alipoulizwa kuhusu mustakabali wake kufuatia sare ya 0-0 ya Morocco na Croatia kwenye mechi yao ya ufunguzi ya Kombe la Dunia siku ya Jumatano, Ziyech alisema: “Hatujui kitakachotokea wakati wa dirisha dogo.Ni soka, hivyo ni vigumu kusema.”
Evening Standard inasema kuwa maoni hayo ya Ziyech yamewaacha mabingwa watetezi wa Serie A Milan wakiwa katika hali ya tahadhari baada ya kujaribu kumsajili mshambuliaji huyo majira ya joto yaliyopita.
Inasemekana kuwa Rossoneri wana hamu ya kumsaini Mchezaji huyo wa Chelsea kwa mkopo wa miezi sita baada ya kumpoteza Alexis Saelemaekers kutokana na jeraha la goti la muda mrefu.

The Standard wanasema Milan pia wanamtaka mshambuliaji wa The Blues Armando Broja lakini wakuu wa Chelsea watakataa mbinu yoyote kwa mchezaji huyo wa Kimataifa wa Albania, ambaye hataki kuondoka.
Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.
BONYEZA HAPA KUCHEZA


