Tunisia Wataitetemesha Uingereza?

Nabil Maaloul ambaye ni kocha wa taifa la Tunisia anakiongoza kikosi chake kuwinda taji la Kombe la Dunia leo hii!

Ikiwa ni mara baada ya wao kuonekana kwenye fainali 3 zilizopita bila ya kushinda mchezo hata mmoja kwenye hatua ya makundi sasa Tunisia wamepenya mpaka makundi!

Wao wamefuzu bila ya kufungwa baada ya kuitandika DR Congo na kwenda Urusi kwa alama kadhaa huku suluhu ya raundi ya mwisho dhidi ya Libya ikithibitisha vya kutosha kuwa kikosi hicho kilichoundwa na wachezaji wengi wanaocheza nyumbani kinastahili kuwika sana!

Hali yao ikoje?
Bado Tunisia wapo imara pamoja na kumkosa kiungo mkongwe Youssef Msakni kwenye michuano hii kutokana na majeraha ya misuli anayougua kwa sasa.

Je, wataweza kuitetemesha Uingereza ya akina Harry Kane?

3 Komentara

    Wapambane tu.

    Jibu

    Wapambene inawezekana

    Jibu

    Inawezekana tu

    Jibu

Acha ujumbe