Ubora FIFA: Tanzania Chini Zaidi, Ujerumani Juu!

Hapo juzi viwango vipya vya ubora wa FIFA vimetangazwa ambapo timu za kandanda za mataifa ya Kenya na Tanzania zimeshuka sana! Hiyo ni orodha ya kila mwezi inayotolewa na FIFA.

Kwa upande wa Afrika ya Mashariki, Harambee Stars ya huko Kenya imeshuka kwa nafasi sita mpaka namba 88 duniani na Taifa Stars wa hapa Tanzania wameporomoka nafasi 5 mpaka namba 125 duniani.

Nao Rwanda wamepanda nafasi 1 mpaka kufika namba 118 huku DR Congo wakiteremka nafasi 14 mpaka namba 42 duniani na Uganda wamepaa nafasi 2 mpaka nafasi ya 71 huku Burundi wakipanda nafasi 3 mpaka namba 129 duniani.

Wanaoongoza
Kwa Africa sasa Misri wanaongoza wakiwa nafasi ya 30 baada ya kushuka nafasi 5 kidunia na Somalia na Eritrea wanakuwa wa mwisho kabisa huku Ujerumani sasa ndiyo taifa bora zaidi kwa kabumbu ulimwenguni!

Hivyo sasa wanawakimbiza Brazil ambao wapo nafasi ya pili. Endelea kuwa nasi hapa kufahamu mengi zaidi.

2 Komentara

    Habar njema

    Jibu

    Tanzania bado sana kimpira

    Jibu

Acha ujumbe