Uchambuzi: Chini ya 23 Wanaotesa Ligi Kubwa

Kuna baadhi ya wachezaji walio na umri wa chini ya miaka 23 wanaofanya mambo makubwa sana katika umri wao. Baadhi ya wachezaji hao wamekuwa nguzo kubwa katika ngazi ya klabu hata timu zao za taifa pia. Tumezoea kuona wachezaji wengi wanafanya vizuri na kuanza kuandika historia zao wanapofikia umri wa jati ya miaka 25 hadi 29, lakini nyota hawa wameanza kukaa kwenye chati za historia mapema zaidi.

Kylian Mbappe

Hadi sasa ana rekodi kubwa kwa kuweza kushinda kombe la dunia akiwa na timu yake ya taifa ya Ufaransa na makombe mengine katika ngazi ya klabu. Hadi sasa katika ligi msimu huu ana idadi ya magoli 17 katika mechi 14 za ligi ya Ufaransa alizozicheza. Kwa aina ya uchezaji wake ana kila sababu ya kufanya vizuri zaidi kwa sasa na hapo mbeleni. Takwimu zake kwa msimu huu zinaridhisha sana kwani amechangia upatikanaji wa magoli 32 ambapo akitoa pasi za magoli 11, na yeye kufumania nyavu mara 21.

Ousmane Dembele

Ni mchezaji wa aina yake anakipiga katika klabu ya Barcelona na umri wake ni miaka 20 tu ila amekuwa nguzo kubwa ndani ya klabu hiyo kwa sasa. Ni mchezaji mwenye uwezo wa pekee linapokuja suala la kuuchezea mpira kutokana na umaridadi wake wa kutumia miguu yote kwa usawa. Hadi sasa ana magoli 13 katika michuano yote aliyocheza. Uwezo wa miguu yake miwili umeweza kumfanya afunge magoli 20 kwa mguu wake wa kulia na namba hiyohiyo kwa mguu wake wa kushoto. Hakika hawa ni tunu ya kutumainiwa ndani ya taifa la Ufaransa.

Jadon Sancho

Anakipiga katika klabu ya Dortmund, amekuwa tishio sio katika kikisi chao tu: bali hata klabu nyingine zinapata shida sana wakati zinapokutana mchezaji huyu, kwa sababu amekuwa akiwapa wakati mgumu hata walinzi akiwa anashambulia. Ni raia wa Uingereza na watu wengi wa taifa lake wanatamani mchezaji huyo angalau angekuwa anacheza ndani ya ligi yao na kuipeperusha zaidi bendera ya taifa lao. Ana umri wa miaka 19 na hadi sasa amefanikiwa kucheza mechi 25. Hizi ni dalili za asubuhi kabisa kwa kikosi cha Uingereza kuimarika zaidi.

Marcus Rashford

Tangu kuondoka kwa Mreno, Mourinho ambaye hakuwa na mapendeleo kumtumia mshambuliaji huyo, nyota yake imeanza kung’aa kwa sasa ndani ya utawala mpya uliopo. Amefanikiwa kufunga magoli matano katika mechi sita alizocheza hivi karibuni; zikiwa ni takwimu nzuri kwa mchezaji huyo raia wa Uingereza.

 

    Itaendelea…

2 Komentara

    Wako vizuri.

    Jibu

    Gud news

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.