UCL: United na City Wavuka!

Baada ya michezo ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya kuanza tena wiki hii sasa tumeshuhudia klabu mbili kubwa zikiwika. Manchester United na Manchester City wavuka! Kwenye misimu 16 ambayo Jose Mourinho ameshiriki mitanange ya UEFA Champions League amewahi kuishia hatua ya makundi mara 1 pekee wakati akiwa na FC Porto mwaka 2000/01.

Jana, baada ya ushindi, amefanikiwa kuingia hatua ya 16 bora. Kwenye kipindi cha maisha yake ameishia hatua ya 16 bora mara 5 tu.

Olympique Lyonnais ilitoka sare ya bao 2 wakicheza na Manchester City ambapo kwa sare hiyo sasa Man City wanaingia kwenye hatua ya mtoano Kundi F huku Lyon na Shaktar wakingoja hatima yao hadi mchezo wa mwisho kundini.

UCL: United na City Wavuka!

2 Komentara

    Zote zipo poa sana

    Jibu

    Timu zote ziko vizuri sana na pia wanajua mpira

    Jibu

Acha ujumbe