Kocha wa Borussia Dortmund Edin Terzic amefurahishwa na droo ya Ligi ya Mabingwa ambapo amepangiwa Chelsea na atakutana na wachezaji wa zamani wa timu hiyo  Pierre-Emerick Aubameyang na Christian Pulisic.

 

Aubameyang na Pulisic Wamsisimua Terzic

Dortmund ilimaliza nafasi ya pili kwenye kundi G  ambalo Manchester City ndiye alishika nafasi ya kwanza katka Ligi ya Mabingwa Ulaya, na baadaye kupangiwa dhidi ya Graham Potter wa The Blues katika droo iliyopangwa hapo jana kwenye hatua ya 16 bora.

Mechi ya kwanza itachezwa Februari 15 kwenye Uwanja wa Signal Iduna Park huku ikiwashuhudia Aubameyang na Pulisic wakirejea katika klabu yao ya zamani, ambapo Aubameyang raia wa Gabon aliifungia mabao 98 kwenye Bundesliga katika kipindi kigumu cha miaka mitano.

Alipoulizwa kuhusu droo hiyo katika mkutano na waandishi wa habari hapo jana  Terzic alisema: “Tukiwa na Chelsea, timu ya juu kutoka Uingereza inatusubiri tukiwa na Aubameyang na Pulisic, wana wachezaji ambao walikuwa nasi hadi miaka michache iliyopita”.

Aubameyang na Pulisic Wamsisimua Terzic

Kocha huyo alisema kuwa pia ni rafiki wa karibu wa Graham Potter na anatazamia kumuona tena, lakini hawatacheza nao sasa ni mpaka Februari. Kuna mengi ya kufanya, kazi nyingi za nyumbani za kufanya, lakini kwa hakika wanatazamia michezo hiyo.

Wapinzani kama hao ndio wanatarajia kupangwa nao kwenye Ligi ya Mabingwa, na wanajaribu kusonga mbele hadi raundi inayofuata. Wakati huo huo Mkurugenzi wa uendeshaji  wa soka wa Chelsea David Barnard amefarijika kutokabiliana na mshambuliaji wa zamani wa Dortmund Erling Haaland, ambaye ameanza vyema huko Uingereza.

Aubameyang na Pulisic Wamsisimua Terzic

Mkurugenzi huyo alisema kuwa wanatazamia kucheza na Dortmund kwasababu itakuwa mara ya kwanza kukutana nao kwenye Ligi ya Mabingwa, itakuwa ya kuvutia, pia walicheza kundi la Manchester City na anatarajia kupata maarifa ya ndani kutoka kwa City kuhusu hilo.

“Ni wazi tuna Pierre kurejea katika moja ya vilabu vyake vya zamani, kwa hivyo tunatazamia.”


AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa