Kocha mkuu wa Liverpool Jurgen Klopp bado ana matumaini ya kutinga hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, licha ya Liverpool kupangwa dhidi ya Real Madrid ambao ndio waliocheza kwenye Fainali msimu uliopita na Majogoo kupoteza kwa 1-0.

 

Klopp Yupo Tayari Kuchuana Dhidi ya Madrid

Liverpool ya Klopp walimaliza nafasi ya pili kwenye kundi A baada ya kuwa sawa pointi na kinara wa kundi hilo Napoli na kutofautiana kwenye magoli ya kufunga na kufungwa, na baada ya droo kupangwa hapo jana wakajikuta wamepangiwa Real Madrid katika hatua ya 16 bora.

Kikosi cha Klopp kimepoteza fainali mbili za Ligi ya Mabingwa dhidi ya Madrid katika misimu mitano iliyopita, lakini Mjerumani huyo anatarajia kukutana tena kwa mara ya pili mfululizo na vijana wa Carlo Ancelotti na kocha huyo akasema kuwa;

Klopp Yupo Tayari Kuchuana Dhidi ya Madrid

“Najua tumecheza na Real Madrid katika fainali kadhaa za hivi majuzi, lakini si mara nyingi vilabu vyetu viwili vimekutana kwa sare ya mikondo miwili, hivyo sasa tunaweza kutarajia hili kutokea.”

Klopp aliongeza kwa kusema kuwa rekodi ya Real ya Ulaya ni bora zaidi na wanafahamu hilo, lakini pia wanajua kwamba rekodi yao sio mbaya pia, na wanajua wana Anfield na wanajua nini maana yake.

Madrid wameshinda mechi zao zote tatu za Ligi ya Mabingwa na Liverpool wakati wakikabiliana nao kama mabingwa wa Ulaya, na mshambuliaji wao wa zamani Emilio Butragueno anaamini kuwa kikosi cha Ancelotti kitakabiliana na shinikizo la kuwa timu ya kubeba taji hilo.

Klopp Yupo Tayari Kuchuana Dhidi ya Madrid

Butragueno alisema kuwa; “Kwa ulimwengu wa soka, itakuwa mechi ya kusisimua kwasababu ya historia ya klabu hizo mbili.”

Alisema pia ni wapinzani wa nguvu sana ambao wamekuwa na utulivu mkubwa katika miaka ya hivi karibuni na kocha mmoja na kundi moja la wachezaji, hivyo inafanya kuwa hatari sana.

Klopp Yupo Tayari Kuchuana Dhidi ya Madrid

“Wakati huo huo, sisi ni mabingwa, na kwa kawaida tutafanya kila linalowezekana ili kufuzu na kurudi kwenye droo ya robo fainali, tunawaamini kabisa wachezaji wetu, wametuonyesha kile wanachoweza katika wakati wa presha kubwa.”


AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa