Kuna wakati mchezaji anaweza kusajiliwa katika kikosi cha klabu fulani kwa malengo ya kufanya vizuri katika kikosi husika au kukiwa na lengo kwamba yale aliyokuwa anayafanya upande wa kwanza yatakuwa mara dufu. Lakini ikaja kuwa kinyume na malengo kwamba mchezaji huyo akashindwa kukaa katika mfumo wa timu hiyo na kupotea kabisa. Miongoni mwa sajili alizowahi kuzifanya Chelsea na akapotea kabisa ni kama zifuatazo;
Radamel Falcao
Usajili huu wa Jose Mourinho ulivunja rekodi baada ya mchezajj huyo kuonekana hafai kabisa ndani ya kikosi hicho baada ya matunda makubwa aliyoyaonesha akiwa na United lakini baada ya kutua kwa miamba hao wa darajani alishindwa kabisa kumudu hata ule ufungaji aliokuwa nao kipindi cha nyuma. Goli pekee aliloifungia klabu hiyo ni lile walipokutana na Crystal Palace pale darajani japo walifungwa katika mchezo ule.
Claudio Pizarro
Pamoja na ubora wake aliokuwa nao ndani ya klabu ya Bayern Munivh kwa kuweza kuchukua kombe la ligi la Ujerumani mara sita akiwa na Bayern Munich, na kombe la klabu bingwa; lakini alishindwa kabisa kuendana na falsafa za klabu ya Chelsea aliposajiliwa na kushindwa kabisa kung’aa ndani ya kikosi hicho kama alivyokua mfungaji bora huko nyuma.
Alexandre Pato
Aliweza kusajiliwa kwa mkopo kutoka Corinthians na kushindwa kabisa kufanya makubwa baada ya kupata nafasi ya kuitumikia klabu hiyo kubwa na yenye historia yake. Katika nyakati zake kikosini hapo alishindwa kuisaidia klabu hiyo kumaliza angalau katika nafasi za juu na kuishia nafasi ya kumi kwenye ligi katika msimu wa 2015/16. Goli pekee alilofunga ilikuwa ni dhidi ya Aston Villa walipopata ushindi wa 4-0.
Alvaro Morata
Hadi sasa ameichezea klabu hiyo michezo 72 akitokea Real Madrid, ndani ya michezo hiyo amefanikiwa kuifungia timu yake magoli 24. Kwa aina ya usajili huu alitakiwa awe amefanya makubwa zaidi ndani ya kikosi hicho lakini, mchezaji huyo amekuwa nje ya malengo ya timu hiyo kwa kupoteza kabisa ule uwezo wa kufumania nyavu uwanjani; na kupoteza nafadi za wazi zinazoonekana. Na kwa mwenendo wake anaweza kutimka klabuni hapo wakati wowote.
Fernando Torres
Ndani ya michezo 172 ndani ya kikosi hicho alifanikiwa kuondoka na magoli 45. Ilionekana ni miongoni mwa usajili mbovu kuwahi kufanywa na klabu hiyo hiyo; hadi kupelekea mchezaji huyo kuondoka klabuni hapo bila kuwa na matunda mazuri kama wengi walivyokuwa wanategemea kutoka kwake.


Njiku
Kweli kabisa sijui tatizo ni mifumo au nini wote wapo poa sana na wanamajina makubwa sana na walimsahau di maria halivyotua manchester united hakufanya vizuri wakamtimua klabuni hapo cjui kwanni
Gabriel
Good news 👍