Ulijua Hii? Ubelgiji Imetengeneza Rekodi Yake!

Hapo jana usiku mara baada ya Ubelgiji kuwatwanga Brazil kwa magoli 2-1 wamefanikiwa kuingia nusu fainali na inakuwa ni mara ya pili kwao kufikia hatua kama hii.

Jikumbushe

Kwa mara ya kwanza na ya mwisho kufikia hatua hiyo ilikuwa ni mwaka 1986 kwenye mitanange iliyofanyika Mexico ambapo kwenye robo fainali, Ubelgiji waliitandika Hispania kwa penalti 5-4 baada ya suluhu ya 1-1 dakika 120 za mchezo wao.

Pia, kwenye nusu fainali wakakatishwa na Argentina pale walipotandikwa magoli 2-0 na katika Kombe la Dunia huko Mexico walioibuka washindi ni Argentina.
Ulijua Hii? Ubelgiji Imetengeneza Rekodi Yake!

2 Komentara

    Kwa sisi mashabiki wa Brazil ilokuwa nizaidi ya maumivu kufungwa na watoto wadogo

    Jibu

    Noma sana hiii

    Jibu

Acha ujumbe