Klabu ya Aston Villa imemteua kocha wa Villarreal Unai Emery kuwa kocha wao mkuu akirithi mikoba ya aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Steven Gerrad mwenye umri wa miaka 42.

 

 Unai Emery Ateuliwa Kuwa Kocha Mkuu wa Aston Villa.

Mhispania huyo atachukua nafasi hiyo Novemba 1 mara tu taratibu zake za kibali cha kazi zitakapokamilika, na hii ina maana kwamba mechi yake ya kwanza kuinoa itakuwa ni dhidi ya Manchester United kwenye ligi kuu ya Uingereza mnamo Novemba 6 .

Unai, ambaye si mgeni katika ligi kuu ya Uingereza, alishawahi kuifundisha Arsenal kutoka mwaka 2018 hadi 2019 na wakati akiwa anaitumikia The Gunners alimaliza katika nafasi ya tano kwenye Ligi na kuwapeleka washika mitutu hao wa London kwenye fainali ya Ligi ya Uropa, ambapo walipoteza dhidi ya Chelsea.

Baada ya kutimuliwa katika viunga vya Emirates, Emery alijiunga na Villarreal mwaka wa 2020 na kufurahia msimu wa kwanza wa kuinoa klabu hiyo, na kukiongoza kikosi hicho kutwaa ubingwa wa Ligi ya Uropa ambapo walicheza fainali dhidi ya United na wakawatoa kwa mikwaju ya penati.

 Unai Emery Ateuliwa Kuwa Kocha Mkuu wa Aston Villa.

Lakini Unai hakuishia hapo aliendeleza ushindi huo kwa kuifikisha Villarreal hatua ya nusu fainali kwenye Ligi ya Mabingwa baada ya kuwatoa Bayern Munich, na hatimae alipofika nusu fainali alikuja kutolewa na Liverpool.

Akitangaza kuondoka, kocha huyo mwenye 50 na Villarreal walitoa taarifa wakisema kuwa; “Villarreal  inapenda kumshukuru Unai Emery kwa kazi alioifanya na inamtakia kila la kheri katika maisha yake ya soka.”

Kabla ya kuwa kocha wa Uingereeza, Emery aliiongoza Sevilla, akishinda Ligi ya Uropa mara tatu. Kisha aliiacha timu ya Uhispania na kwenda Paris Saint-Germain na kuwaongoza Psg kunyakua taji la Ligue 1 mnamo 2017-18 kabla ya kujiunga na Arsenal msimu huo wa joto.

 Unai Emery Ateuliwa Kuwa Kocha Mkuu wa Aston Villa.

Sasa, Emery anachukua timu ya Aston Villa ambayo kwa sasa inashika nafasi ya 15 kwenye msimamo wakiwa pointi tatu juu ya eneo la kushuka daraja,  baada ya kuifunga Brentford 4-0 siku ya Jumapili.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa