Baada ya kukamilisha usajili wa kiungo wa Real Madrid Carlos Casemiro klabu ya Man United imehamishia nguvu kwa kiungo wa pembeni raia wa Brazil anayekipiga katika klabu ya Ajax ya nchini Uholanzi Anthony Santos.united, United Na Wabrazili Damudamu., Meridianbet
United inajaribu kuingia sokoni kutafuta winga mwenye makali ambae ataweza kuleta matokeo chanya katika safu yao ya ushambuliaji,kwasababu wengi waliopo katika nafasi hiyo ndani ta klabu wameonekana kupoteza makali hivo mwalimu Eric Ten Hag ameona aingie sokoni na mchezaji anaeonekana kutolewa macho ni winga huyo anayefanya vizur katika klabu ya Ajax.
Imeripotiwa klabu ya Man United ilipeleka ofa ya euro milioni 80 kama dau la kumuhitaji mchezaji huyo lakini ofa hiyo ilikataliwa.
 Huku upande wa mchezaji ukionekana kulazimisha ofa hiyo kupokelewa na klabu yake ya Ajax, Akihitaji kuungana na mwalimu wake wa zamani ndani ya klabu hiyo. Inaelezwa siku ya ijumaa nyota huyo wa kibrazili hakuonekana kujumuika mazoezini ma wachezaji wenzake hivo kuonesha kila dalili winga huyo anahitaji usajili wake kukamilika ili aweze kujiunga na Manchester United.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa