Wakati timu mbalimbali zikiendelea na mchakato wa usajili, Manchester United bado inahaha kwenye mipango. Frankie De Jong ni changamoto.

United inapambana kuiwania sahihi ya usajili wa De Jong akitokea FC Barcelona. Mkataba wake na Barca haujaisha lakini, klabu hiyo inaaminika kuwa kwenye mpango wa kupunguza nyota wao kadhaa ili kuweka sawa vitabu vyao vya mahesabu. Ukata ni hali inayoitikisa Barca kwa muda sasa, mauzo ya wachezaji pekee ndio sehemu ya kuponea.

Kizungumkuti kwenye usajili wa De Jong kipo kwa mchezaji mwenyewe, Barca hawana tatizo na kumuuza mchezaji huyo kama tu, thamani wanayoitaka itafikiwa na timu inayomuhitaji. Kwa hali ilivyo, ni Manchester United pekee ndio inayoonesha nia thabiti ya kumuhitaji kiungo huyo. Tatizo ni, United haichezi Ligi ya Mabingwa msimu ujao na, kiungo huyo hataki kwenda kwenye timu isiyoshiriki mashindano hayo.

Usajili, Usajili wa De Jong Kizungumkuti, Meridianbet
Ten Hag na De Jong walipokuwa Ajax.

Japokuwa maongezi kati ya United na Barca yanaonesha matumaini (kulingana na ripoti mbalimbali), bado United inakazi ya ziada kumshawishi De Jong kutua Old Trafford licha ya uwepo wa Erik Ten Hag ambaye ni kocha aliyemnoa na kumfanya kuwa mchezaji nyota kwenye ulimwengu wa soka.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

 

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa